Mkataba wa Hali Bom ya Kazi Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na CHODAWU

New2

MKATABA WA HALI BORA YA KAZI BAINA YA HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA (TANAPA) AMBAYE KWA MADHUMUNI YA MAKUBALIANO HAYA ATAJULIKANA KAMA MWAJIRI KWA UPANDE MMOJA NA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA HIFADHI, HOTELI, MAJUMBANI, HUDUMA ZA JAMII NA USHAURI (CHODAWU) AMBAYE KWA MADHUMUNI YA MAKUBALIANO HAYA ATAJULIKANA KAMA CHAMA KWA UPANDE WA PILI

KWA KUWA pande zote zimekubaliana kuwa na uhusiano baina yao, uhusiano huo utatoa haki na majukumu kwa kila upande,

NA

KWA KUWA pande zote zinatambua misingi ya uhuru wa kujumuika na haki ya kushiriki katika majadiliano ya pamoja,

NA

KWA KUWA kila upande unatambua haja ya kuwepo mfumo fanisi utakaohakikisha kuwepo kwa uhusiano wa haki katika ajira na haja ya kutatua migogoro baina yao kwa amani kwa njia ya mashauriano na majadiliano,

NA

KWA KUWA kila upande unatambua haja ya kuwa na uhusiano mzuri na amani mahali pa kazi,

HIVYO BASI pande zote zinakubaliana kama ifuatavyo:-

1.0 MUDA WA MKATABA

1.1Muda wa mkataba huu utakuwa miaka mitatu toka tarehe ya kusainiwa baada ya kupata ridhaa ya Msajili wa Hazina. Mkataba huu unaweza kufanyiwa marejeo (review) pale ambapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo au miezi sita kabla ya muda wa mkataba kuisha.

1.2 Endapo muda wa Mkataba utaisha na ule uliorejewa haujakamilika, mkataba wa awali utaendelea kutumika mpaka pale ule uliorejewa utakapokamilika.

2.0 AJIRA

2.1 Taratibu za ajira zitazingatia Sheria za nchi, Kanuni za Utumishi, barua za ajira na nyaraka mbalimbali zitakazokuwa zikitolewa mara kwa mara na Bodi ya Wadhamini au Serikali.

2.2 Nafasi za kazi zinapotokea na kutangazwa kwenye vyombo vya habari, nakala ya tangazo hilo ipelekwe kwa wakuu wote wa Hifadhi kwa njia iliyo rahisi ikiwa ni pamoja na barua pepe na nukushi na kuwekwa kwenye mbao za matangazo sehemu za kazi.

3.0 KUACHISHWA KAZI

Mtumishi anaweza kuachishwa kazi na mwajiri kwa kuzingatia Sheria za nchi, Kanuni na Taratibu zilizopo.

4.0 SAA ZA KAZI

4.1 Saa za kazi, saa za ziada (Overtime), siku za Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu (Public Holidays) zitatambulika kwa mujibu wa Sheria za nchi.

4.2 Malipo ya saa za ziada na siku za Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu yatalipwa kwa kuzingatia viwango vya Serikali vya "Extra Duty Allowance" ambavyo vitaboreshwa na kuwa shilingi 10,000/= kwa "Junior Staff" na shilingi 15,000/= kwa "Senior Staff" katika ngazi ya Principal kwa siku. Hata hivyo viongozi kuanzia ngazi ya mshahara ya G.10 na kuendelea hawastahili malipo hayo.

4.3 Malipo ya saa za ziada yatafanyika kunapokuwepo kazi inayotaka kukamilishwa nje ya wakati wa kazi. Idhini ya kazi ya ziada lazima iwe kwa maandishi kutoka kwa kiongozi/ mkuu wa Hifadhi wa kazi.

4.4 Viongozi wawaruhusu watumishi kupumzika kila inapowezekana badala ya kulipwa kwa kufanya kazi saa za ziada.

5.0 KUPUNGUZWA KAZI (REDUNDANCY)

Mtumishi atakayepunguzwa kazi kwa sababu zaidi ya kuyumba kwa uchumi

na mbali na makosa ya kinidhamu atastahili:-

5.1 Kulipwa mishahara kwa viwango vifuatavyo;

i. Miaka mitano (5) kurudi chini watalipwa mishahara ya miezi 24.

ii. Miaka zaidi ya mitano (5) hadi miaka kumi (10) watalipwa mishahara ya miezi 36.

iii. Miaka zaidi ya kumi (10) watalipwa mishahara ya miezi 48.

5.2 Kulipwa Mkono wa Heri (Golden Handshake) kiasi cha shilingi milioni kumi na tano (15,000,000/ =).

5.3 Usafirishiwa familia na mizigo yake hadi nyumbani kwake kiasi cha tani 2 kwa ngazi za mishahara TAN 01-TAN 05 na G1 - G5 na tani 4 kwa ngazi za G6 — G13.

6.0 VIFO NA MAZISHI

6.1 Mtumishi atakapofariki au kufiwa gharama za mazishi zitakuwa kama zilivyoainishwa katika Kanuni za Utumishi.

6.2 Mtumishi anapofariki au kufiwa atasindikizwa na watumishi wasiopungua watano.

6.3 Rambirambi italipwa kwa mujibu wa waraka uliopo na kwa jinsi utakavyoboreshwa mara kwa mara.

7.0 MPANGO WA MAFUNZO (TRAINING PROGRAMME)

Mafunzo yatashughulikiwa kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi na Sera ya

Mafunzo na kwa kuzingatia mahitaji na vipaumbele vya Shirika.

8.0 KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA

8.1 Mishahara ya watumishi wa Shirika itaendelea kuboreshwa kulingana na hali ya mapato ya Shirika itakavyokua.

Mkataba wa Hali Bora ya Kazi Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na CHODAWU 

8.2 Kima cha chini cha mshahara kinacholipwa wakati wa kusainiwa mkataba huu kitaendelea kulipwa na kuboreshwa kwa kadri hali ya kifedha ya Mwajiri itakavyoruhusu.

9.0 MAFAO YA KUSTAAFU

9.1. Mwajiri atawajibika kuandaa mafao ya mtumishi anayekaribia ia kustaafu miezi sita kabla ya kustaafu na kumpa taarifa mtumishi husika kwa maandishi.

9.2. Mtumishi anao wajibu wa kumkumbusha mwajiri kwa maandishi miezi sita kabla ya tarehe ya kustaafu.

9.3. Mtumishi atakayestaafu atastahili kulipwa Mkono wa Heri (Golden Handshake) kiasi cha shilingi milioni kumi (10,000,000/=) kwa atakayestaafu kwa hiari (kuanzia miaka 55) na shilingi milioni kumi na tano (15,000,000/=) kwa atakayestaafu kwa mujibu wa Sheria.

9.4. Mtumishi atakayestaafu kwa mujibu wa Sheria au kwa hiari au kufariki kabla ya kufikisha umri wa kustaafu atalipwa mishahara ya miezi 48 kama mafao ya kustaafu kutoka kwenye mfuko maalum.

9.5. Mtumishi atakayestaafu kwa ugonjwa atastahili kulipwa mafao yaliyoainishwa kwenye kifungu Na. 9.4 na Mkono wa Heri kiasi cha shilingi milioni kumi (10,000,000/ =) pamoja na stahili nyingine.

10.0 LIKIZO YA MWAKA (ANNUAL LEAVE)

10.1 Likizo ya mwaka ya mtumishi itakuwa ni siku 28 kwa mujibu wa sheria za ajira na mahusiano kazini Na. 6 1. ya mwaka 2004.

11.0 MALIPO YA LIKIZO

11.1 Mtumishi na familia yake (Watoto wanne na mke/mume) atastahili malipo ya nauli ya likizo ya kila mwaka.

11.2 Malipo ya nauli ya likizo yatamhusu mume/mke na watoto wanne bila kuzingatia kama mume/ mke anafanya kazi sehemu au taasisi nyingine. 

11.3 Malipo hayo ya likizo yatastahili watoto wa mtumishi wenye umri chini ya miaka kumi na nane (18) au umri usiozidi miaka ishirini na moja (21) iwapo watoto hao wanasoma shule au chuo na baada ya kupokea uthibitisho.

12.0 LIKIZO YA UZAZI

Watumishi watastahili likizo ya Uzazi kwa mujibu wa sheria za kazi na kanuni za Utumishi za TANAPA.

13.0 LIKIZO KWA AJILI YA MASOMO

Likizo kwa ajili ya masomo zitazingatia Kanuni za Utumishi za TANAPA.

14.0 MATIBABU

Mwajiri atagharamia matibabu kwa mtumishi na familia yake kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi.

15.0 KUUMIA KAZINI

15.1 Mtumishi atakayeumia kazini na kupata ulemavu wa kudumu na baada ya kupokea uthibitisho kutoka kwa mganga wa Serikali aliye na Mamlaka hiyo atastahili malipo ya fidia kama ifuatavyo;

i. Atakayepoteza viungo kama sikio, jicho, vidole TZS 5,000,000/=.

ii. Atakayepoteza mkono au mguu TZS 10,000,000/=.

iii. Atakayepooza (paralysis), kupoteza miguu yote, macho yote, au mkono na mguu au kupoteza uhai (familia yake italipwa)- TZS 15,000,000/=.

15.2 Familia ya mtumishi inapopatwa na ajali hifadhini (mfano kudhuriwa na wanyama) atastahili nusu ya malipo ya mtumishi ya kuumia au kufariki kazini.

16.0 MALIPO NA UBORESHAJI WA TUZO NA POSHO MBALIMBALI

Tuzo na posho zinazolipwa kwa watumishi wakati wa kusainiwa mkataba huu zitaendelea kutumika na kuboreshwa kadri hali ya kifedha ya Shirika itakavyokuwa nzuri.

17.0 SARE ZA WATUMISHI

Mwajiri atatoa jozi moja ya sare kamili kwa mwaka kwa watumishi kwa kuzingatia mazingira halisi ya kazi.

18.0 TARATIBU ZA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO

Taratibu za kushughulikia migogoro sehemu za kazi zitazingatia Sheria husika za nchi.

19.0 MALIPO KWA WATEGEMEZI BAADA YA MTUMISHIKUFARIKI

Mtumishi anapofariki familia ya marehemu italipwa mishahara ya mtumishi ya miezi mitano (5) na itaruhusiwa kukaa kwenye nyumba ya Shirika si zaidi ya miezi minne au italipwa posho ya pango kwa miezi minne (4).

20.0 MAKAZI BORA KWA WATUMISHI

Mwajiri ataboresha vitendea kazi pamoja na makazi ya watumishi kulingana na hali ya kifedha itakavyoruhusu.

21.0 TUZO YA UHIFADHI

Utaratibu wa sasa wa kulipa Tuzo ya Uhifadhi (Conservation Award) kwa kuzingatia mshahara wa mtumishi katika Shirika uendelee kila Shirika litakapofikia malengo na kupata hati safi toka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). Tuzo ya Uhifadhi italipwa kama mshahara wa mwezi wa kumi na tatu wa mtumishi katika mwaka husika wa fedha baada ya malengo ya Shirika kufikiwa kwa mwaka huo.

22.0 UHAMISHO

Uhamisho wa watumishi utashughulikiwa kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi.

23.0 UHAMISHO WA MUDA

Uhamisho wa muda kwenda kituo kingine cha kazi kwa kazi maalum utazingatia Kanuni za Utumishi.

24.0 MICHEZO, SHEREHE NA TAFRIJA

24.1 Mwajiri atahakikisha kuwepo kwa michezo, sherehe na tafrija mbalimbali mahali pa kazi.

24.2 Kutakuwepo na kamati ya ustawi wa jamii kwa kila Hifadhi na Makao Makuu ambayo itakuwa na majukumu ya kuratibu, kuandaa na kupanga mipango ya michezo, sherehe na tafrija kwa ajili ya watumishi.

24.3 Mwajiri atawajibika kugharamia vifaa vya michezo na burudani mbalimbali mahali pa kazi kulingana na bajeti itakayokuwa imeidhinishwa na Bodi ya Wadhamini na kuhamasisha watumishi kushiriki.

25.0 KUPANDISHWA CHEO

25.1Mwajiri anaweza kumpandisha cheo mtumishi kwa kuzingatia vigezo vya Shirika kwa mujibu wa Miundo ya Utumishi (Schemes of Service), pamoja na kuwepo nafasi husika.

25.2 Mwajiri atawajibika kumjulisha mtumishi sababu za kutompandisha cheo kwa maandishi pindi mtumishi huyo anapokuwa amekidhi vigezo vya kupandishwa cheo kiutendaji, kinidhamu na uzoefu.

25.3 Mtumishi atakayefaulu mafunzo ya muda mrefu atastahili kupewa nyongeza ya mshahara wake kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi.

26.0 MIKOPO KWA WATUMISHI

26.1 Mwajiri atadhamini watumishi wake kukopa kutoka Taasisi za kifedha.

26.2 Shirika litakapotoa mikopo, mikopo hiyo haitakuwa na riba na itarejeshwa ndani ya muda utakaokuwa umewekwa,

26.3 Mshahara wa mtumishi hautaruhusiwa kukatwa kwa kiwango kitakachozidi robo ya mshahara (net salary), na Shirika halitahusika kwa lolote endapo mtumishi ataacha kuwa mtumishi yaani kwa kuacha kazi, kifo au kustaafu.

27.0 WATUMISHI WA MUDA NA WA MKATABA MAALUMU

Ajira zote zitazingatia Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Kanuni za Utumishi na Nyaraka (circulars) zitakazokuwa zikitolewa na Serikali au Bodi ya Wadhamini.

28.0 SHULE ZA AWALI (NURSERY SCHOOLS)

Mwajiri atawezesha uanzishaji wa shule za awali katika kila Hifadhi pale inapohitajika na kwa mujibu wa Sheria na Taratibu za Serikali.

29.0 TAFSIRI ZA NYARAKA MBALIMBALI

29.1 Nyaraka mbalimbali zinazohusu watumishi na maslahi yao zitaandikwa kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza.

29.2 Nyaraka hizo zitawekwa bayana na mwajiri atahakikisha kuwa zinawafikia watumishi mapema iwezekanavyo.

30.0 MATUKIO YA KIJASIRI

Matukio yote ya kijasiri yatakayofanywa na mtumishi kama vile kuokoa mali za shirika, maisha ya binadamu na mali zao yatatambuliwa na Mwajiri sanjari na kupewa tuzo maalum.

31.0 NYONGEZA YA MSHAHARA YA MWAKA (ANNUAL SALARY INCREMENT)

31.1Mwajiri atawajibika kutoa nyongeza ya mshahara ya mwaka kwa watumishi kwa kuzingatia Kanuni za Utumishi.

31.2 Mwajiri hatalazimika kumlipa nyongeza ya mshahara ya mwaka mtumishi ambaye utendaji wake wa kazi utathibitika kuwa hauridhishi na atapaswa kumjulisha kwa maandishi.

32.0 KALENDA YA MWAKA YA SHIRIKA

Mwajiri ataandaa kalenda inayoonyesha shughuli na matukio mbalimbali vikiwemo vikao katika shirika kwa kipindi cha mwaka mzima (k.m. mabaraza ya wafanyakazi), na kuiweka wazi kwa watumishi wote.

33.0 MIUNDO YA UTUMISHI (SCHEMES OF SERVICE)

Mabadiliko ya Miundo ya Utumishi yatashirikisha Chama.

34.0 SERA YA UKIMWI (HIV /AIDS CONTROL POLICY)

Sera ya kuzuia na kudhibiti UKIMWI itazingatiwa kama ilivyopitishwa na Mwajiri.

35.0 KAMATI ZA AFYA NA USALAMA KAZINI

Kutakuwa na Kamati ya Afya na Usalama Kazini katika kila Hifadhi na Makao Makuu ambayo itasimamia na kutekeleza Sheria ya Afya na Usalama Kazini ya mwaka 2003.

36.0 AHADI KWA SHIRIKA (COMMITMENTS)

36.1 Watumishi wote watatakiwa kuzingatia Sheria za nchi, Kanuni na Taratibu za Shirika katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

36.2 Kila mtumishi atashiriki kikamilifu katika kulinda maliasili, wageni (watalii) na mali za Shirika pamoja na mapato na matumizi ya Shirika.

36.3 Kila mtumishi anao wajibu wa kutoa mawazo endelevu ili kuendeleza fursa za uwekezaji ili kukuza tija.

36.4 Mkataba huu unatambua kuwa kuna haki na wajibu katika utumishi wa Slairika ili malengo makuu yaani Uhifadhi, Utalii na Utumishi yaweze kufikiwa.

36.5 Kila mtumishi atatekeleza malengo yake ya kazi kwa mujibu wa mfumo wa "OPRAS".

36.6 Kila mtumishi atahakikisha kuwa ujangili unadhibitiwa, kutokomezwa na kuwa yeye mwenyewe hashiriki katika vitendo vya ujangili au katika njia itakayofanikisha uhalifu ndani ya Hifadhi. Pia mtumishi ana wajibu wa kutoa taarifa kwa vyombo husika anapopata ufahamu wa mipango ya kufanya uhalifu ndani ya Hifadhi.

36.7 Watumishi watawajibika kuvaa mavazi yenye kuzingatia maadili ya Taifa.

36.8Ni marufuku mtumishi kutumia madawa ya kulevya nje na ndani ya sehemu za kazi au aina yoyote ya kilevi sehemu za kazi.

37.0 UKIUKAJI NA USITISHAJI WA MKATABA

37.1 Endapo upande wowote utakiuka masharti ya msingi ya mkataba huu, upande utakaoathirika utakuwa na haki ya kupeleka malalamiko hayo kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

37.2 Endapo upande wowote utashindwa kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa mkataba huu, upande mwingine unayo haki ya kupeleka malalamiko hayo kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi iwapo upande unaolalamikiwa hautakuwa umeanza kushughulikia bila sababu za msingi jambo linalolalamikiwa ndani ya siku kumi na tano (15) za kazi kuanzia tarehe ya kupokea taarifa ya lalamiko kutoka upande mwingine.

CHODAWU

Kwa niaba ya mwajiri:

Kwa niaba ya Chama:

GENERAL SECRETARY

Mkataba wa Hali Bom ya Kazi Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na CHODAWU - 2014

Start date: → 2014-01-01
End date: → Not specified
Ratified by: → Ministry
Ratified on: → Not yet ratified
Name industry: → Hospitality, catering, tourism
Name industry: → Camping grounds, recreational vehicle parks and trailer parks
Public/private sector: → In the private sector
Concluded by:
Name company: →  TANAPA
Names trade unions: →  Conservation, Hotel, Domestic and Allied Workers’ Union (CHODAWU)

TRAINING

Training programmes: → Yes
Apprenticeships: → No
Employer contributes to training fund for employees: → No

SICKNESS AND DISABILITY

Provisions regarding return to work after long-term illness, e.g. cancer treatment: → 
Paid menstruation leave: → No
Pay in case of disability due to work accident: → Yes

WORK AND FAMILY ARRANGEMENTS

Maternity paid leave: → 13 weeks
Job security after maternity leave: → No
Prohibition of discrimination related to maternity: → No
Prohibition to oblige pregnant or breastfeeding workers to perform dangerous or unhealthy work: → 
Workplace risk assessment on the safety and health of pregnant or nursing women: → 
Availability of alternatives to dangerous or unhealthy work for pregnant or breastfeeding workers: → 
Time off for prenatal medical examinations: → 
Prohibition of screening for pregnancy before regularising non-standard workers: → 
Prohibition of screening for pregnancy before promotion: → 
Facilities for nursing mothers: → No
Employer-provided childcare facilities: → Yes
Employer-subsidized childcare facilities: → No
Monetary tuition/subsidy for children's education: → Yes

WORKING HOURS, SCHEDULES AND HOLIDAYS

Paid annual leave: → 28.0 days
Paid annual leave: → 4.0 weeks
Provisions on flexible work arrangements: → 

WAGES

Wages determined by means of pay scales: → No
Adjustment for rising costs of living: → 

Wage increase

Once only extra payment

Once only extra payment due to company performance: → Yes

Premium for overtime work

Premium for overtime work: → TZS 10000.0 per hour overtime

Premium for Sunday work

Premium for Sunday work: → TZS 10000.0 per Sunday

Meal vouchers

Meal allowances provided: → No
Free legal assistance: → 
Loading...