MKATABA WA HIARI NA HALI BORA ZA KAZI No: 4 WA MWAKA 2016 - 2017 BAINA YA GREEN RESOURCES LIMITED (GRL) & TANZANIA PLANTATION AND AGRICULTURAL WORKERS UNION (TPAWU)

New2

No: 4

ii) Mfanyakazi wa ngazi ya juu ya uongozi (Senior Management Employee), pamoja na Mameneja wa Mashambani (Plantation Managers).

1.6 Tafasiri ya Wataalamu na Menejimenti:

1.6.1 Wataalamu: Mfanyakazi mtaalamu aliyeajiriwa na kampuni na ambaye Tanzania siyo nchi yake ya asili.

1.6.2 Mfanyakazi wa ngazi ya juu ya uongozi: Mfanyakazi ambaye kulingana na nafasi ya mfanyakazi huyo, i) anatengeneza sera kwa niaba ya mwajiri na ii) anaruhusiwa kuingia mikataba ya hiari kwa niaba ya mwajiri.

2. UFAFANUZI

2.1 GREEN RESOURCES LIMITED ni kampuni inayohusika na upandaji miti, kutunza mazingira na kuuza hewa ukaa.

2.2 CHAMA- ina maana chama cha wafanyakazi wa mashambani na kilimo. Tanzania Plantations and Agricultural Workers Union (TPAWU).

23 SERI KALI - ina maana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2.4 VIONGOZI WA CHAMA - ina maana Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Katibu wa Kanda na Katibu wa sehemu, pamoja na viongozi wa kuchaguliwa.

2-5 KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA: - ina maana mshahara wa kuanzia wafanyakazi wa GREEN RESOURCES LIMITED.

2.6 ADA ZA CHAMA: - ina maana ada ya Chama ambayo Mwajiri atawasilisha ada hizo kwa Chama mara baada ya kulipa mishahara.

3. MKAKATI WA KUPAMBANA NA VVU/ UKIMWI

3.1 Tunakubaliana kwamba Mwajiri kwa kushirikiana na Chama itafuata sera ya Ukimwi ya Taifa katika masuala yote yanayohusu VVU/UKIMWI.

3.2. Kwamba Mwajiri kwa kushirikiana na matawi ya Chama mahali pa kazi tutafanya jitihada za makusudi kuona kwamba wafanyakazi wanapata elimu na ufahamu juu ya njia za kujikinga na VVU/UKIMWI.

5. LIKIZO

5.1 Tumekubaliana kwamba likizo zitatolewa kwa mujibu wa sheria ya kazi.

5.2 Tumekubaliana kwamba Mwajiri atamlipia nauli mfanyakazi ikiwa ni pamoja na Mke/Mume na watoto wasiozidi wanne (4) wenye umri chini ya miaka 18 au 21 kama wanasoma; aliowaandikisha na kuwasilisha vyeti vya kuzaliwa vya watoto na ndoa kwa Mwajiri.

5.3 Tumekubaliana kwamba Mwajiri atalipa nauli hiyo tajwa mpaka Makao Makuu ya Wilaya ya mahali Mfanyakazi alipoandikisha wakati wa ajira yake kwa Mwajiri. Viwango vya nauli vitakuwa sawa na viwango vinavyotangazwa mara kwa mara na SUMATRA (Surface and Marine Transport Regulatory Authority) kwa ajili ya mabasi aina ya "semi luxury" kwa kutumia njia (route) fupi kwa kadri itavyowezekana.

5.4 LIKIZO YA UGONJWA

Tumekubaliana kwamba likizo ya ugonjwa itatolewa kwa mujibu wa sheria ya kazi.

5.5 LIKIZO YA UZAZI

5.5.1 Tumekubaliana kwamba Mfanyakazi mwanamke atakayejifungua atapewa likizo ya siku mia moja (100) zenye malipo.

5.5.2 Tumekubaliana kwamba baba mzazi wa mtoto atakayezaliwa atapewa likizo kulingana na mujibu wa sheria ya kazi ili kutoa fursa kwa wazazi wote kushirikiana kulea mtoto.

5.6 LIKIZO YA MSIBA

Tumekubaliana kwamba Mfanyakazi atakayefiwa na baba, mama mzazi, mke/mume au mtoto aliowaandikisha na kuwasilisha vyeti vyao kwa Mwajiri, atapewa likizo ya siku saba (7) zenye malipo.

8. KAMPUNI KUUZWA, KU1NGIA UBIA AU KUYUNJIKA

Tumekubaliana kwamba endapo kampuni itauzwa, kuingia ubia au kuvunjika, menejimenti na TPAWU watajadiliana na kukubaliana juu ya haki za Wafanyakazi, kwa kufuata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa kwenye Sheria ya Kazi.

9. KUUMIA KAZINI

Mfanyakazi atakayeumia kazini atalipwa kutoka kwenye mfuko wa taifa wa mafao ya kuumia kazini (Workmen’s Compensation Fund, Act. 20 of 2008), ambapo mwajiri huchangia kila mwezi kulingana na sheria.

10. MATIBABU

Tumekubaliana kwamba Wafanyakazi pamoja na familia zao walizoziandikisha kwa Mwajiri wataendelea kutibiwa kwa utaratibu uliowekwa na kampuni.

11. NYUMBA

11.1 WAFANYAKAZI WA MASHAMBANI

Tumekubaliana kwamba kwa kadri itakavyowezekana Mwajiri atawapatia Wafanyakazi wa mashambani nyumba na Wafanyakazi hao watakatwa kiasi cha fedha kulingana na thamani ya nyumba kwa viwango vilivyoainishwa hapa chini:-

1. Vyumba vitatu (3) vya kulala na sebule ya peke yake - TZS. 30,000/=

2. Vyumba viwili (2) vya kulala na sebule ya peke yake - TZS. 20,000/=

3. Chumba kimoja (1) cha kulala na sebule ya peke yake - TZS. 10,000/=

4. Vyumba viwili (2) vya kulala, sebule ya pamoja, choo na bafu - TZS. 8,500/=

5. Chumba kimoja (1) cha kulala, sebule ya pamoja, choo na bafu - TZS. 5,000/=

6. Chumba kimoja (1) na choo/ bafu ya pamoja - TZS. 3,000/=

7. Mabweni (kuanzia watu wawili (2) - wanne (4) - TZS. 0/

Pamoja na haya, Mwajiri kwa kuzingatia hali ya maisha ya mashambani, haswa masuala ya kijamii, atawapatia wafanyakazi asilimia kumi na tano (15%) ya mshahara kama kodi ya ayummba.

12.5 Kwamba Mfanyakazi atakayefiwa na wazazi wake wa kumzaa yaani baba au mama mzazi, Mwajiri atatoa rambirambi ya Shilingi Laki Moja tu (TZS. 100,000/=).

13. POSHO NJE YA KITUO CHA KAZI

Tumekubaliana kwamba Mfanyakazi atakayesafiri kikazi ndani ya nchi atalipwa posho kwa kila siku atakayokuwa nje ya kituo chake cha kazi kulingana na viwango vya kampuni. Ieleweke kwamba pale ambapo Mwajiri atatoa malazi na chakula kwa Mfanyakazi atakayekuwa nje ya kituo chake cha kazi basi posho tajwa hapo juu haitalipwa.

14. ELIMU KWA WAFANYAKAZI

14.1 Tumekubaliana kwamba Mwajiri anawatia moyo Wafanyakazi wote kujiendeleza kielimu na pia inatoa fursa kwa Wafanyakazi wote na hasa wale wa ngazi ya chini ili wapate taaluma stahiki. Wafanyakazi watakaopendekezwa na Mwajiri kwenda kusomea fani ambazo ni mahitaji ya Mwajiri, basi watapewa likizo na Mwajiri atagharamia masomo kwa utaratibu ufuatao:-

a) Kwamba Mwajiri atamkata Mfanyakazi kiasi kisichozidi asilimia hamsini (50%) ya mshahara kamili. Mwajiri atahakikisha kwamba kiasi kitakachobaki kwa Mfanyakazi baada ya makato si chini ya kima cha chini cha mshahara cha wakati husika.

b) Kwamba ili Mwajiri aweze kumruhusu Mfanyakazi alieomba kwenda masomoni, basi Mfanyakazi atatakiwa kutoa taarifa miezi sita (6) kabla ya likizo tajwa kwa Mwajiri.

c) Kwamba Mfanyakazi atakayetaka kwenda masomoni ni lazima awe amemtumikia Mwajiri kwa muda usiopungua miaka mitatu (3) toka aajiriwe.

d) Kwamba Mfanyakazi atakayekuwa masomoni atatakiwa kuripoti na kuendelea na kazi kila mara apatapo likizo.

e) Kwamba Mfanyakazi baada ya kumaliza masomo yake atawajibika kumtumikia Mwajiri kwa muda usiopungua ule aliokuwa masomoni.

Kwamba Mfanyakazi atakayeacha kazi kabla ya muda uliotajwa kipengele 14.1 (e), wajibika kumrudishia Mwajiri ada ya masomo pamoja na mshahara aliokuwa

17. CHAKULA WAKATI WA KAZI

Tumekubaliana kwamba, wakati wote Mwajiri atatoa chakula cha mchana kwa wafanyakazi wote, na cha jioni kwa Wafanyakazi wanaoishi kwenye makambini. Mwajiri atajitahidi kutoa mlo kamili na hakutakuwa na chakula cha aina moja wakati wote.

18. MFANYAKAZI/WAFANYAKAZI BORA

Tumekubaliana kwamba kutakuwa na utaratibu wa kuchagua Wafanyakazi bora kila mwaka ambao watatunukiwa vyeti vya heshima na Chama kwenye sherehe za Wafanyakazi yaani Mei Mosi. Wafanyakazi hao watachaguliwa na uongozi wa kila Shamba kwa kushirikiana na Kamati za Matawi ya Chama.

a) Kwamba kila Shamba/Tawi litatoa Mfanyakazi bora kila mwaka wakati wa Mei Mosi.

b) Kwamba Wafanyakazi bora watakaochaguliwa kutoka kila Shamba/Tawi; watashindanishwa; na Mfanyakazi atakayekuwa bora zaidi atapelekwa kushindanishwa kwenye ngazi ya Mkoa.

c) Kwamba Mwajiri atatoa vifaa mbalimbali kama zawadi kwa wafanyakazi bora vyenye thamani ya Shilingi Laki Mbili tu (TZS 200,000/=).

d) Kwamba Mwajiri atatoa vifaa vyenye thamani ya Shilingi Laki Tatu tu (TZS 300,000/=) kwa Mfanyakazi atakayeibuka mshindi ngazi ya Mkoa.

e) Kwamba endapo Mfanyakazi atakuwa bora ngazi ya Taifa, Mwajiri atajadiliana na uongozi wa Chama juu ya zawadi gani itolewe.

f) Kwamba zawadi za Wafanyakazi bora zitatolewa siku ya sherehe na siyo baada ya sherehe.

19. JUMAMOSI ZA KAZI

Imekubalika kwamba hakutakuwa na jumamosi za kazi na zisizo za kazi kwa Wafanyakazi wa mashambani. Jumamosi zote zitakuwa za kazi.

JINA:

SAHIHI:

WADHIFA: MENEJA PENDESHAJI

Mkataba wa Hiari na Hali Bora za Kazi Baina ya Green Resources Limited (GRL) & Tanzania Plantation and Agricultural Workers Union (TPAWU) - 2016

Start date: → 2016-01-01
End date: → 2017-12-31
Ratified by: → Ministry
Ratified on: → 2016-01-01
Name industry: → Agriculture, forestry, fishing
Name industry: → Forestry and logging
Public/private sector: → In the private sector
Concluded by:
Name company: →  Green Resources Limited
Names trade unions: →  TPAWU

TRAINING

Training programmes: → Yes
Apprenticeships: → No
Employer contributes to training fund for employees: → No

SICKNESS AND DISABILITY

Provisions regarding return to work after long-term illness, e.g. cancer treatment: → 
Paid menstruation leave: → No
Pay in case of disability due to work accident: → Yes

WORK AND FAMILY ARRANGEMENTS

Maternity paid leave: → 14.3 weeks
Maternity paid leave restricted to 100 % of basic wage
Job security after maternity leave: → No
Prohibition of discrimination related to maternity: → No
Prohibition to oblige pregnant or breastfeeding workers to perform dangerous or unhealthy work: → 
Workplace risk assessment on the safety and health of pregnant or nursing women: → 
Availability of alternatives to dangerous or unhealthy work for pregnant or breastfeeding workers: → 
Time off for prenatal medical examinations: → 
Prohibition of screening for pregnancy before regularising non-standard workers: → 
Prohibition of screening for pregnancy before promotion: → 
Facilities for nursing mothers: → No
Employer-provided childcare facilities: → No
Employer-subsidized childcare facilities: → No
Monetary tuition/subsidy for children's education: → No
Paternity paid leave: → Not specified days

WAGES

Wages determined by means of pay scales: → No
Adjustment for rising costs of living: → 

Meal vouchers

Meal vouchers provided: → Yes
Meal allowances provided: → No
Free legal assistance: → 
Loading...